1 Wafuatao ni watu wa mkoani waliotoka utumwani ambao Nebukadneza mfalme wa Babuloni aliwapeleka mateka Babuloni, wakarudi mjini Yerusalemu na nchini Yuda. Kila mtu alirudi mjini kwake.
2 Viongozi wao walikuwa Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana.Ifuatayo ni idadi ya watu wote wa koo za Israeli waliorudi kutoka uhamishoni:
3 Wa ukoo wa Paroshi: 2,172;
4 wa ukoo wa Shefatia: 372;
5 wa ukoo wa Ara: 775;
6 wa ukoo wa Pahath-moabu, yaani wazawa wa Yeshua na Yoabu: 2,812;
7 wa ukoo wa Elamu: 1,254;
8 wa ukoo wa Zatu: 945;
9 wa ukoo wa Zakai: 760;
10 wa ukoo wa Bani: 842;
11 wa ukoo wa Bebai: 623;
12 wa ukoo wa Azgadi: 1,222;
13 wa ukoo wa Adonikamu: 666;
14 wa ukoo wa Bigwai: 2,056;
15 wa ukoo wa Adini: 454;
16 wa ukoo wa Ateri, yaani Hezekia: 98;
17 wa ukoo wa Besai: 323;
18 wa ukoo wa Yora: 112;
19 wa ukoo wa Hashumu: 223;
20 wa ukoo wa Gibari: 95.
21 Watu wa mji wa Bethlehemu: 123;
22 wa mji wa Netofa: 56;
23 wa mji wa Anathothi: 128;
24 wa mji wa Azmawethi: 42;
25 wa mji wa Kiriath-yearimu, wa Kefira na wa Beerothi: 743;
26 wa mji wa Rama na wa Geba: 621;
27 wa mji wa Mikmashi: 122;
28 wa mji wa Betheli na Ai: 223;
29 wa mji wa Nebo: 52;
30 wa mji wa Magbishi: 156;
31 wa mji wa Elamu wa pili: 1,254;
32 wa mji wa Harimu: 320;
33 wa mji wa Lodi, Hadidi na wa Ono: 725;
34 wa mji wa Yeriko: 345;
35 wa mji wa Senaa: 3,630.
36 Ifuatayo ni idadi ya makuhani waliorudi kutoka uhamishoni: Makuhani wa ukoo wa Yedaya, waliokuwa wazawa wa Yeshua: 673;
37 wa ukoo wa Imeri: 1,052;
38 wa ukoo wa Pashuri: 1,247;
39 wa ukoo wa Harimu: 1,017.
40 Walawi wa ukoo wa Yeshua na wa Kadmieli, wazawa wa Hodavia waliorudi kutoka uhamishoni walikuwa 74.
41 Waimbaji (wazawa wa Asafu), walikuwa 128.
42 Walinzi (wazawa wa Shalumu, wa Ateri, wa Talmoni, wa Akubu, wa Hatita na wa Shobai), walikuwa 139.
43 Koo za watumishi wa hekalu waliorudi kutoka uhamishoni zilikuwa: Ukoo wa Siha, wa Hasufa, wa Tabaothi,
44 ukoo wa Kerosi, wa Siaha, wa Padoni,
45 ukoo wa Lebana, wa Hagaba, wa Akubu,
46 ukoo wa Hagabu, wa Shamlai, wa Hanani,
47 ukoo wa Gideli, wa Gahari, wa Reaya,
48 ukoo wa Resini, wa Nekoda, wa Gazamu,
49 ukoo wa Uza, wa Pasea, wa Besai,
50 ukoo wa Asna, wa Meunimu, wa Nefisimu,
51 ukoo wa Bakbuki, wa Hakufa, wa Harhuri,
52 ukoo wa Basluthi, wa Mehida, wa Harsha,
53 ukoo wa Barkosi, wa Sisera, wa Tema,
54 ukoo wa Nezia na wa Hatifa.
55 Koo za wazawa wa watumishi wa Solomoni waliorudi kutoka uhamishoni zilikuwa, ukoo wa Sotai, wa Hasoferethi, wa Perudha,
56 ukoo wa Yaala, wa Darkoni, wa Gideli,
57 ukoo wa Shefatia, wa Hatili, wa Pokereth-hasebaimu na wa Ami.
58 Nao watumishi wote wa hekalu na wazawa wa watumishi wa Solomoni waliorudi kutoka uhamishoni walikuwa watu 392.
59 Watu wa miji ifuatayo, pia walirudi: Wa mji wa Tel-mela, wa Tel-harsha, wa Kerubu, wa Adani na wa Imeri, ila hawakuweza kuthibitisha kuwa walikuwa wazawa wa Waisraeli.
60 Wao walikuwa watu wa ukoo wa Delaya wa Tobia na wa Nekoda, jumla watu 652.
61 Watu wa koo zifuatazo za makuhani pia walirudi: Ukoo wa Habaya, wa Hakosi na wa Barzilai. Huyo Barzilai alikuwa ameoa binti Barzilai wa Gileadi, naye pia akaitwa Barzilai.
62 Hao walitafuta orodha yao katika kumbukumbu za koo, lakini hawakuonekana humo. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kushika ukuhani kwani walihesabiwa kuwa najisi.
63 Mtawala akawaambia kuwa hawaruhusiwi kushiriki chakula kitakatifu sana, mpaka awepo kuhani atakayeweza kutoa kauli ya Urimu na Thumimu.
64 Watu wote waliorudi kutoka uhamishoni jumla yao ilikuwa 42,360;
65 mbali na hao, kulikuwa na watumishi wanaume na wanawake 7337; na walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake, wote 200.
66 Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245,
67 ngamia 435, na punda 6,720.
68 Watu hao waliotoka uhamishoni, walipofika kwenye nyumba ya Mwenyezi-Mungu mjini Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa koo hizo walitoa matoleo ya hiari ili kusaidia ujenzi wa nyumba ya Mungu katika Yerusalemu.
69 Walitoa kila mtu kadiri ya uwezo wake kwa ajili ya kazi hii. Jumla ya matoleo hayo ilikuwa kilo 500 za dhahabu, kilo 2,800 za fedha na mavazi 100 kwa ajili ya makuhani.
70 Basi, makuhani, Walawi na baadhi ya watu wengine wakaanza kuishi mjini Yerusalemu na katika vitongoji vyake. Nao waimbaji, walinzi wa hekalu na watumishi wa hekalu wakaanza kuishi katika miji yao; Waisraeli wote waliishi katika miji yao.