5 Wakazi wa Samaria watatetemekakwa sababu ya ndama wa huko Betheli.Watu wake watamwombolezea ndama huyo,hata makuhani wanaomwabudu watamlilia;kwani fahari ya ndama huyo imeondolewa.
6 Kinyago hicho kitapelekwa Ashuru,kama ushuru kwa mfalme mkuu.Watu wa Efraimu wataaibishwa,Waisraeli watakionea aibu kinyago chao.
7 Mfalme wa Samaria atachukuliwa,kama kipande cha mti juu ya maji.
8 Mahali pa kuabudia vilimani pa Aweni,dhambi ya Waisraeli, pataharibiwa.Miiba na magugu vitamea katika madhabahu zao.Nao wataiambia milima, “Tufunikeni”na vilima, “Tuangukieni!”
9 Enyi Waisraeli,nyinyi mmetenda dhambi tangu kule Gibea,na bado mnaendelea.Hakika vita vitawaangamiza hukohuko Gibea.
10 Nitawajia watu hawa wapotovu na kuwaadhibu;watu wa mataifa watakusanyika kuwashambulia,watakapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao nyingi.
11 Efraimu ni ndama aliyefundishwa vizuri,akapenda kupura nafaka.Lakini sasa shingo yake nzuri nitaifunga nira.Yuda atalima kwa jembe yeye mwenyewe,naam, Yakobo atakokota jembe la kupalilia.