1 Sasa sikilizeni enyi wakuu wa wazawa wa Yakobo,sikilizeni, enyi watawala wa wazawa wa Israeli!Nyinyi ndio mnaopaswa kujua mambo ya haki.
2 Lakini nyinyi mnachukia mema na kupenda maovu.Mnawachuna ngozi watu wangu,na kubambua nyama mifupani mwao.
3 Mnajilisha kwa nyama ya watu wangumnawachuna ngozi yao,mnaivunjavunja mifupa yao,na kuwakatakata kama nyama ya kupika,kama nyama ya kutia ndani ya chungu.
4 Wakati unakuja ambapo mtamlilia Mwenyezi-Mungu,lakini yeye hatawajibu.Atauficha uso wake wakati huo,kwa sababu mmetenda mambo maovu.
5 Mwenyezi-Mungu asema hivikuhusu manabii wanaowapotosha watu wake;manabii ambao hutabiri amani wakipewa kitu,lakini huwatishia watu kwa vita wasipopewa kitu:
6 “Kwenu manabii kutakuwa usiku bila maono,kutakuwa giza kwenu bila ufunuo.Kwenu manabii kutakuchwa,mchana utakuwa giza kwenu.”
7 Mabingwa wa maono watafedheheka,mafundi wa kubashiri wataaibishwa;wote watafunga midomo yao,maana hawatapata jibu lolote kutoka kwa Mungu.
8 Lakini kwa upande wangu,nimejazwa nguvu na roho ya Mwenyezi-Mungu;nimejaliwa kujua haki na kuwa na uwezoniwatangazie wazawa wa Yakobo kosa lao,niwaambie Waisraeli dhambi yao.
9 Sikieni jambo hili enyi viongozi wa wazawa wa Yakobo,sikilizeni, enyi watawala wa Waisraeli:Nyinyi mnachukia mambo ya hakina kupotosha mambo ya adili.
10 Nyinyi mnajenga mji wa Siyoni kwa damu,naam, mji wa Yerusalemu kwa dhuluma.
11 Waamuzi hufanya kazi yao kwa rushwa,makuhani wake hufundisha kwa malipo,manabii hutabiri kwa fedha.Hata hivyo hujidai kumtegemea Mwenyezi-Mungu,wakisema, “Mwenyezi-Mungu, si yupo pamoja nasi?Hatutapatwa na madhara yoyote!”
12 Haya! Kwa sababu yenu,Siyoni utalimwa kama shamba,Yerusalemu utakuwa magofu,nao mlima wa hekalu utakuwa msitu.