1 Kisha Bildadi, Mshuhi, akajibu:
2 “Mungu ni mwenye uwezo mkuu,watu wote na wamche.Yeye huweka amani mpaka juu kwake mbinguni.
3 Nani awezaye kuhesabu majeshi yake?Ni nani asiyeangaziwa na mwanga wake?
4 Mtu awezaje basi, kuwa mwadilifu mbele ya Mungu?Binadamu tu awezaje kujidai kuwa safi?
5 Kwake Mungu, hata mwezi haungai vya kutosha;nyota nazo si safi mbele yake;
6 sembuse mtu ambaye ni mdudu,binadamu ambaye ni buu tu!”