20 Mtu mwovu huwa na uchungu siku zake zote,Hata hesabu ya miaka aliyowekewa mwenye kuonea.
21 Sauti za utisho zi masikioni mwake;Katika kufanikiwa kwake mtekaji nyara atamjia juu yake;
22 Yeye hasadiki kwamba atarudi kutoka gizani,Naye hungojewa na upanga;
23 Hutanga-tanga ili apate chakula, akisema, Ki wapi?Ajua kwamba siku ya giza i tayari karibu yake;
24 Mateso na dhiki humtia hofu;Humshinda kama vile mfalme aliye tayari kwa vita;
25 Kwa kuwa amenyosha mkono wake juu ya Mungu,Na kuendelea kwa kiburi kinyume cha Mwenyezi;
26 Humshambulia na shingo ngumu,Kwa mafundo makubwa ya ngao zake;