1 Lakini sasa hao walio wadogo wangu hunifanyia mzaha,Ambao baba zao niliwadharau hata kuwaweka na mbwa wa kundi langu.
2 Naam, uwezo wa mikono yao utanifaa nini?Watu ambao nguvu zao zimekoma.
3 Wamekonda kwa uhitaji na njaa;Huguguna nchi kavu, penye giza la ukiwa na uharibifu.
4 Hung’oa mboga ya chumvi kwenye kichaka;Na mizizi ya mretemu ni chakula chao.