27 Sayuni itakombolewa kwa hukumu, na waongofu wake kwa haki.
28 Lakini kuharibika kwao wakosao nao wenye dhambi kutatokea wakati mmoja, nao wamwachao BWANA watateketezwa.
29 Kwa maana watatahayarika kwa sababu ya mialoni mliyoitamani, nanyi mtaaibishwa kwa sababu ya bustani mlizozichagua.
30 Maana mtakuwa kama mwaloni ambao majani yake yakauka, na kama bustani isiyo na maji.
31 Na mtu hodari atakuwa kama makumbi, na kazi yake kama cheche ya moto; nao watawaka pamoja, wala hapana atakayewazima.