7 kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.
8 Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.
9 Tazama, mambo ya kwanza yamekuwa, nami nayahubiri mambo mapya; kabla hayajatokea nawapasheni habari zake.
10 Mwimbieni BWANA wimbo mpya,Na sifa zake tokea mwisho wa dunia;Ninyi mshukao baharini, na vyote vilivyomo,Na visiwa, nao wakaao humo.
11 Jangwa na miji yake na ipaze sauti zao,Vijiji vinavyokaliwa na Kedari;Na waimbe wenyeji wa Sela,Wapige kelele toka vilele vya milima.
12 Na wamtukuze BWANA,Na kutangaza sifa zake visiwani.
13 BWANA atatokea kama shujaa;Ataamsha wivu kama mtu wa vita;Atalia, naam, atapiga kelele;Atawatenda adui zake mambo makuu.