4 Inua macho yako, utazame pande zote;Wote wanakusanyana; wanakujia wewe;Wana wako watakuja kutoka mbali.Na binti zako watabebwa nyongani.
5 Ndipo utakapoona na kutiwa nuru,Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka;Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia,Utajiri wa mataifa utakuwasilia.
6 Wingi wa ngamia utakufunika,Ngamia vijana wa Midiani na Efa;Wote watakuja kutoka Sheba;Wataleta dhahabu na uvumba;Na kuzitangaza sifa za BWANA.
7 Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako,Kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia;Watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali,Nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu.
8 Ni nani hawa warukao kama wingu,Na kama njiwa waendao madirishani kwao?
9 Hakika yake visiwa vitaningojea,Na merikebu za Tarshishi kwanza,Ili kuleta wana wako kutoka mbali,Na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao,Kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wako,Kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli,Kwa kuwa amekutukuza wewe.
10 Na wageni watajenga kuta zako,Na wafalme wao watakuhudumu;Maana katika ghadhabu yangu nalikupiga,Lakini katika upendeleo wangu nimekurehemu.