11 Busara itakulinda;Ufahamu utakuhifadhi.
12 Ili kukuokoa na njia ya uovu,Na watu wanenao yaliyopotoka;
13 Watu waziachao njia za unyofu,Ili kuziendea njia za giza;
14 Wafurahio kutenda mabaya;Wapendezwao na upotoe wa waovu;
15 Waliopotoka katika njia zao;Walio wakaidi katika mapito yao.
16 Ili kuokoka na malaya,Naam, malaya mwenye kubembeleza kwa maneno yake;
17 Amwachaye rafiki wa ujana wake,Na kulisahau agano la Mungu wake.