4 Ndipo nikasema, Hakika, hawa ni maskini; ni wajinga hawa; maana hawaijui njia ya BWANA, wala hukumu ya Mungu wao;
5 nitawaendea watu wakubwa, nami nitasema nao; kwa maana hao wanaijua njia ya BWANA, na hukumu ya Mungu wao. Bali hawa kwa nia moja wameivunja nira, na kuvikata vifungo.
6 Basi, kwa hiyo, simba atokaye mwituni atawaua, mbwa-mwitu wa jioni atawateka, chui ataivizia miji yao, kila mtu atokaye humo atararuliwa vipande vipande; kwa sababu makosa yao ni mengi, na kurudi nyuma kwao kumezidi.
7 Nawezaje kukusamehe? Watoto wako wameniacha mimi, na kuapa kwa hao ambao si miungu; nilipokuwa nimewashibisha chakula, walizini, wakakutana wengi pamoja katika nyumba za makahaba.
8 Walikuwa kama farasi walioshiba wakati wa asubuhi; kila mmoja akalia kwa kutamani mke wa mwenzake.
9 Je! Nisiwapatilize kwa sababu ya mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu, je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii?
10 Pandeni juu ya kuta zake mkaharibu, lakini msiharibu kabisa; ondoeni matawi yake; kwa maana si yake BWANA.