14 Kwa kuwa BWANA hatawatupa watu wake,Wala hutauacha urithi wake,
15 Maana hukumu itairejea haki,Na wote walio wanyofu wa moyo wataifuata.
16 Ni nani atakayesimamaKwa ajili yangu juu ya wabaya?Ni nani atakayenisaidiaJuu yao wafanyao maovu?
17 Kama BWANA asingalikuwa msaada wangu,Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya.
18 Niliposema, Mguu wangu unateleza;Ee BWANA, fadhili zako zilinitegemeza.
19 Katika wingi wa mawazo ya moyoni mwangu,Faraja zako zaifurahisha roho yangu.
20 Je! Kiti cha udhalimu kishirikiane nawe,Kitungacho madhara kwa njia ya sheria?