3 Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mmegundua kwamba Bwana ni mwema.”
4 Basi, mwendeeni Bwana! Yeye ndiye jiwe hai lililokataliwa na watu; lakini mbele ya Mungu ni jiwe teule na la thamani kubwa.
5 Mwendeeni yeye kama mawe hai mkajengeke na kuwa nyumba ya kiroho ambamo mtatumikia kama makuhani watakatifu, kutolea tambiko za kiroho zenye kumpendeza Mungu kwa njia ya Yesu Kristo.
6 Maana Maandiko Matakatifu yasema:“Tazama! Naweka jiwe huko Siyoni,jiwe la msingi, teule na la thamani.Mtu atakayemwamini huyo hataaibishwa.”
7 Kwenu nyinyi mnaoamini, jiwe hilo ni la thamani kubwa; lakini kwa wale wasioamini,“Jiwe walilolikataa waashi,sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.”
8 Tena Maandiko yasema:“Jiwe hilo ni jiwe la kujikwaa,mwamba wa kuwaangusha watu.”Watu hujikwaa kwa sababu hawauamini ule ujumbe; na ndivyo walivyopangiwa tangu mwanzo.
9 Lakini nyinyi ni ukoo mteule, makuhani wa Mfalme, taifa takatifu; watu wake Mungu mwenyewe, mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya Mungu aliyewaiteni kutoka gizani, akawaingizeni katika mwanga wake mkuu.