1 Usimkemee mwanamume mzee, bali msihi kama vile angekuwa baba yako. Watendee vijana wa kiume kama ndugu zako,
2 wanawake wazee kama mama zako, na vijana wa kike kama dada zako, kwa usafi wote.
3 Waheshimu wanawake wajane walio wajane kweli.
4 Lakini mjane aliye na watoto au wajukuu, hao wanapaswa kujifunza kutimiza wajibu wao wa kidini kwa jamaa zao wenyewe na hivyo kuwalipa wazazi wao na wazee wao, kwani hilo ni jambo la kupendeza mbele ya Mungu.
5 Mwanamke mjane kweli, asiye na mtu wa kumsaidia, amemwekea Mungu tumaini lake na huendelea kusali na kumwomba msaada usiku na mchana.
6 Lakini mwanamke ambaye huishi maisha ya anasa, huyo amekufa, ingawa yu hai.
7 Wape maagizo haya, wasije wakawa na lawama.