4 wakanywa pia kinywaji kilekile cha kiroho, maana walikunywa kutoka ule mwamba wa kiroho uliowafuata; mwamba huo ulikuwa Kristo mwenyewe.
5 Hata hivyo, wengi wao hawakumpendeza Mungu, na maiti zao zilisambazwa jangwani.
6 Sasa, mambo hayo yote ni mfano tu kwetu; yanatuonya sisi tusitamani ubaya kama wao walivyotamani.
7 Msiwe waabudu sanamu kama baadhi yao walivyokuwa; kama yasemavyo Maandiko: “Watu waliketi kula na kunywa, wakasimama kucheza.”
8 Wala tusizini kama baadhi yao walivyozini, wakaangamia siku moja watu 23,000.
9 Tusimjaribu Bwana kama baadhi yao walivyomjaribu, wakauawa na nyoka.
10 Wala msinungunike kama baadhi yao walivyonungunika, wakaangamizwa na Mwangamizi!