5 Hata hivyo, wengi wao hawakumpendeza Mungu, na maiti zao zilisambazwa jangwani.
6 Sasa, mambo hayo yote ni mfano tu kwetu; yanatuonya sisi tusitamani ubaya kama wao walivyotamani.
7 Msiwe waabudu sanamu kama baadhi yao walivyokuwa; kama yasemavyo Maandiko: “Watu waliketi kula na kunywa, wakasimama kucheza.”
8 Wala tusizini kama baadhi yao walivyozini, wakaangamia siku moja watu 23,000.
9 Tusimjaribu Bwana kama baadhi yao walivyomjaribu, wakauawa na nyoka.
10 Wala msinungunike kama baadhi yao walivyonungunika, wakaangamizwa na Mwangamizi!
11 Basi, mambo hayo yaliyowapata wao ni kielelezo kwa wengine, na yaliandikwa ili kutuonya sisi ambao mwisho wa nyakati unatukabili.