36 Je, mnadhani neno la Mungu limetoka kwenu nyinyi au kwamba limewajieni nyinyi peke yenu?
37 Kama mtu yeyote anadhani kwamba yeye ni mjumbe wa Mungu au kwamba anacho kipaji cha Roho, na ajue kwamba haya ninayowaandikia nyinyi ni amri ya Bwana.
38 Lakini mtu asiyetambua hayo, basi, mtu asimjali mtu huyo.
39 Hivyo basi, ndugu zangu, mnapaswa kuwa na hamu ya kutangaza ujumbe wa Mungu; lakini msimkataze mtu kusema kwa lugha ngeni.
40 Lakini yote yafanyike kwa heshima na kwa utaratibu.