7 Basi, habari za imani yenu zimetutia moyo katika taabu na mateso yetu yote,
8 kwani sasa tunaishi kweli ikiwa nyinyi mnasimama imara katika kuungana na Bwana.
9 Sasa tunaweza kumshukuru Mungu wetu kwa ajili yenu. Tunamshukuru kwa furaha tuliyo nayo mbele yake kwa sababu yenu.
10 Tunazidi kumwomba Mungu usiku na mchana kwa moyo wetu wote ili atupatie fursa ya kuwaoneni uso kwa uso ili tuweze kurekebisha chochote kilichopungua katika imani yenu.
11 Tunamwomba Mungu, Baba yetu mwenyewe, na Bwana wetu Yesu, atutayarishie njia ya kuja kwenu.
12 Bwana awawezeshe nyinyi kupendana na kuwapenda watu wote zaidi na zaidi, kama vile sisi tunavyowapenda nyinyi.
13 Hivyo ataiimarisha mioyo yenu, nanyi mtakuwa wakamilifu na watakatifu mbele ya Mungu na Baba yetu wakati Bwana wetu Yesu atakapokuja pamoja na wote walio wake.