6 Alipomwona Yesu kwa mbali, alimkimbilia, akamwinamia
7 akisema kwa sauti kubwa, “Una nini nami, wewe Yesu Mwana wa Mungu aliye juu? Kwa jina la Mungu, nakusihi usinitese!” (
8 Alisema hivyo kwa kuwa Yesu alikuwa amemwambia, “Pepo mchafu, mtoke mtu huyu.”)
9 Basi, Yesu akamwuliza, “Jina lako nani?” Naye akajibu, “Jina langu ni ‘Jeshi,’ maana sisi tu wengi.”
10 Kisha akamsihi Yesu asiwafukuze hao pepo katika nchi ile.
11 Kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe malishoni kwenye mteremko wa mlima.
12 Basi, hao pepo wakamsihi, “Utupeleke kwa hao nguruwe, tuwaingie.”