1 Siku moja, saa tisa alasiri, Petro na Yohane walikuwa wakienda hekaluni, wakati wa sala.
2 Wakati huo watu walikuwa wanambeba mtu mmoja kiwete tangu kuzaliwa. Watu hao walikuwa wakimweka huyo mtu kila siku kwenye mlango wa hekalu uitwao “Mlango Mzuri,” ili aombe chochote kwa wale waliokuwa wakiingia hekaluni.
3 Alipowaona Petro na Yohane wakiingia hekaluni, aliwaomba wampe chochote.
4 Petro na Yohane walimkodolea macho, naye Petro akamwambia, “Tutazame!”
5 Naye akawageukia, akitazamia kupata kitu kutoka kwao.