43 Nyinyi mlikibeba kibanda cha mungu Moloki,na sanamu ya nyota ya mungu wenu Refani.Sanamu mlizozifanya ndizo mlizoabudu.Kwa sababu hiyo nitawapeleka mateka mbali kupita Babuloni!’
44 Kule jangwani babu zetu walikuwa na lile hema la maamuzi. Lilitengenezwa kama Mungu alivyomwambia Mose alifanye; nakala kamili ya kile alichooneshwa.
45 Kisha babu zetu walilipokezana wao kwa wao mpaka wakati wa Yoshua, walipoinyakua ile nchi kutoka kwa mataifa ambayo Mungu aliyafukuza mbele yao. Hapo lilikaa mpaka nyakati za Daudi.
46 Daudi alipata upendeleo kwa Mungu, akamwomba Mungu ruhusa ya kumjengea makao yeye aliye Mungu wa Yakobo.
47 Lakini Solomoni ndiye aliyemjengea Mungu nyumba.
48 “Hata hivyo, Mungu Mkuu haishi katika nyumba zilizojengwa na binadamu; kama nabii asemavyo:
49 ‘Bwana asema:Mbingu ni kiti changu cha enzina dunia ni kiti changu cha kuwekea miguu.