11 Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake.Huo ulikuwa wakati Wayahudi walipopelekwa uhamishoni Babuloni.
12 Baada ya Wayahudi kupelekwa uhamishoni Babuloni,Yekonia alimzaa Shealtieli,Shealtieli alimzaa Zerubabeli,
13 Zerubabeli alimzaa Abiudi,Abiudi alimzaa Eliakimu,Eliakimu alimzaa Azori,
14 Azori alimzaa Zadoki,Zadoki alimzaa Akimu,Akimu alimzaa Eliudi,
15 Eliudi alimzaa Eleazari,Eleazari alimzaa Mathani,Mathani alimzaa Yakobo,
16 Yakobo alimzaa Yosefu, mumewe Maria mama yake Yesu aitwaye Kristo.
17 Basi, kulikuwa na vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi mpaka Wayahudi walipochukuliwa mateka Babuloni, na vizazi kumi na vinne tangu kuchukuliwa mateka mpaka wakati wa Kristo.