1 Siku hiyohiyo, Yesu alitoka katika ile nyumba, akaenda na kuketi kando ya ziwa.
2 Makundi makubwa ya watu yalimzunguka hata Yesu akapanda mashuani, akaketi. Watu wote walisimama kwenye ukingo wa ziwa,
3 naye Yesu akawaambia mambo mengi kwa mifano.“Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.
4 Alipokuwa akipanda mbegu, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.
5 Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi. Zikaota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina.
6 Jua lilipochomoza, ziliteketea; na kwa kuwa mizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka.
7 Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga.