13 Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa.
14 Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote.
15 “Basi, mtakapoona ‘Chukizo Haribifu lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake),
16 hapo, walioko Yudea na wakimbilie milimani.
17 Aliye juu ya paa la nyumba yake asishuke kuchukua kitu nyumbani mwake.
18 Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake.
19 Ole wao kina mama waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo!