15 “Basi, mtakapoona ‘Chukizo Haribifu lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake),
16 hapo, walioko Yudea na wakimbilie milimani.
17 Aliye juu ya paa la nyumba yake asishuke kuchukua kitu nyumbani mwake.
18 Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake.
19 Ole wao kina mama waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo!
20 Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe siku za baridi au siku ya Sabato!
21 Maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka leo, wala haitapata kutokea tena.