48 Lakini kama mtumishi mbaya akijisemea moyoni: ‘Bwana wangu amekawia kurudi,’
49 kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, akaanza kula na kunywa pamoja na walevi,
50 bwana wake atakuja siku asiyoitazamia na saa asiyoijua.
51 Atamwadhibu vibaya na kumweka kundi moja na wanafiki. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.