5 Maana wengi watatokea wakisema kila mmoja kwamba yeye ndiye Kristo nao watawapotosha watu wengi.
6 Mtasikia juu ya vita na fununu za vita; lakini msifadhaike, maana hayo hayana budi kutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
7 Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi.
8 Yote hayo ni kama mwanzo wa maumivu ya kujifungua mtoto.
9 “Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa sababu ya jina langu.
10 Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana.
11 Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi.