9 “Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa sababu ya jina langu.
10 Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana.
11 Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi.
12 Kwa sababu ya ongezeko la uhalifu, upendo wa watu wengi utafifia.
13 Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa.
14 Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote.
15 “Basi, mtakapoona ‘Chukizo Haribifu lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake),