5 Lakini wakaamua jambo hilo lisifanyike wakati wa sikukuu, kusije kukatokea ghasia kati ya watu.
6 Yesu alipokuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni, aitwaye Mkoma,
7 mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya thamani kubwa, alimjia pale mezani alipokuwa amekaa kula chakula, akammiminia hayo marashi kichwani.
8 Wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Ya nini hasara hii?
9 Marashi haya yangaliweza kuuzwa kwa bei kubwa, maskini wakapewa hizo fedha.”
10 Yesu alitambua mawazo yao, akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mama? Yeye amenitendea jambo jema.
11 Maskini mnao daima pamoja nanyi, lakini mimi sitakuwapo pamoja nanyi daima.