1 Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi.
2 Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa.
3 Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”
4 Yesu akamjibu, “Imeandikwa:‘Mtu haishi kwa mkate tu,ila kwa kila neno asemalo Mungu.’”
5 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu,