3 Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”
4 Yesu akamjibu, “Imeandikwa:‘Mtu haishi kwa mkate tu,ila kwa kila neno asemalo Mungu.’”
5 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu,
6 akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa:‘Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako;watakuchukua mikononi mwao,usije ukajikwaa kwenye jiwe.’”
7 Yesu akamwambia, “Imeandikwa pia:‘Usimjaribu Bwana, Mungu wako.’”
8 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,
9 akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama ukipiga magoti na kuniabudu.”