5 Kuna Bwana mmoja, imani moja na ubatizo mmoja;
6 kuna Mungu mmoja na Baba wa wote, ambaye yuko juu ya wote, afanya kazi katika yote na yuko katika yote.
7 Kila mmoja wetu amepewa neema kadiri ya kipimo alichojaliwa na Kristo.
8 Kama yasemavyo Maandiko:“Alipopaa mbinguni juu kabisa,alichukua mateka;aliwapa watu zawadi.”
9 Basi, inaposemwa: “Alipaa juu,” ina maana gani? Maana yake ni kwamba, kwanza alishuka mpaka chini kabisa duniani.
10 Basi, huyo aliyeshuka hapa duniani ndiye aliyepaa juu ya mbingu zote apate kuujaza ulimwengu.
11 Ndiye aliyewapa watu zawadi: Wengine aliwajalia wawe mitume, wengine manabii, wengine wawe waeneza Injili, wengine wachungaji na waalimu.