17 Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana.
18 Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho Mtakatifu.
19 Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Bwana nyimbo na Zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu.
20 Mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
21 Kila mmoja amstahi mwenzake kwa sababu ya heshima mliyo nayo kwa Kristo.
22 Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana.
23 Maana mume anayo mamlaka juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na mamlaka juu ya kanisa; naye Kristo mwenyewe hulikomboa kanisa, mwili wake.