3 Msifanye chochote kwa moyo wa fitina au kwa majivuno ya bure; muwe na unyenyekevu nyinyi kwa nyinyi, na kila mmoja amwone mwenzake kuwa bora kuliko yeye mwenyewe.
4 Pasiwe na mtu anayetafuta faida yake mwenyewe tu bali faida ya mwenzake.
5 Muwe na msimamo uleule aliokuwa nao Kristo Yesu:
6 Yeye, kwa asili alikuwa daima Mungu;lakini hakufikiri kwamba kule kuwa sawa na Munguni kitu cha kungangania kwa nguvu.
7 Bali, kwa hiari yake mwenyewe,aliachilia hayo yote, akajitwalia hali ya mtumishi,akawa sawa na wanadamu,akaonekana kama wanadamu.
8 Alijinyenyekesha na kutii mpaka kufa,hata kufa msalabani.
9 Kwa sababu hiyo Mungu alimkweza juu kabisa,akampa jina lililo kuu kuliko majina yote.