3 Je, nyinyi ni wajinga kiasi hicho? Nyinyi mlianza yote kwa msaada wa Roho, je, mnataka sasa kumaliza kwa nguvu zenu wenyewe?
4 Je, mambo yale yote yaliyowapata nyinyi yamekuwa bure tu? Haiwezekani!
5 Je, Mungu huwajalia Roho na kutenda miujiza kati yenu ati kwa sababu mnatimiza yanayotakiwa na sheria, ama kwa sababu mnasikia Injili na kuiamini?
6 Chukueni kwa mfano habari za Abrahamu: Yeye alimwamini Mungu, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu.
7 Sasa basi, jueni kwamba watu wenye kumwamini ndio walio watoto halisi wa Abrahamu.
8 Maandiko Matakatifu yalionesha kabla kwamba Mungu atawafanya watu wa mataifa kuwa waadilifu kwa njia ya imani. Hivyo Maandiko Matakatifu yalitangulia kumtangazia Abrahamu Habari Njema: “Katika wewe mataifa yote yatabarikiwa.”
9 Basi, wale walio na imani wanabarikiwa pamoja na Abrahamu aliyeamini.