14 Kwake yeye tunakombolewa, yaani dhambi zetu zinaondolewa.
15 Kristo ni mfano wa Mungu asiyeonekana;ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
16 Maana kwake vitu vyote viliumbwakila kitu duniani na mbinguni,vitu vinavyoonekana na visivyoonekana:Wenye enzi, watawala, wakuu na wenye nguvu.Vyote viliumbwa kwake na kwa ajili yake.
17 Yeye alikuwako kabla ya vitu vyote;vyote huendelea kuwako kwa uwezo wake.
18 Yeye ni kichwa cha mwili wake, yaani kanisa;yeye ni chanzo cha uhai wa huo mwili.Yeye ndiye mwanzo,mzaliwa wa kwanza aliyefufuliwa kutoka kwa wafu,ili awe na nafasi ya kwanza katika vitu vyote.
19 Maana Mungu alipenda utimilifu wake wote uwe ndani yake.
20 Kwake vitu vyote vilipatanishwa na Mungu:Na kwa damu yake msalabani akafanya amanina vitu vyote duniani na mbinguni.