20 Enyi watoto, watiini wazazi wenu daima maana hiyo humpendeza Bwana.
21 Nanyi wazazi, msiwachukize watoto wenu, la sivyo watakata tamaa.
22 Enyi watumwa, watiini wakuu wenu wa kidunia katika mambo yote, na si tu wakati wanapowatazama kwa kuwa mnataka kujipendekeza kwao; ila fanyeni hivyo kwa moyo wote, kwa sababu ya kumcha Bwana.
23 Kila mfanyacho, fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu.
24 Kumbukeni kwamba atawapeni tuzo lile alilowawekea watu wake. Mtumikieni Kristo Bwana!
25 Atendaye mabaya atalipwa kufuatana na ubaya wake; Mungu hana ubaguzi.