6 Basi, tunavyo vipaji mbalimbali kadiri ya neema tuliyopewa. Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri ya imani yake.
7 Mwenye kipaji cha utumishi na atumikie. Mwenye kipaji cha kufundisha na afundishe.
8 Mwenye kipaji cha kuwafariji wengine na afanye hivyo. Mwenye kumgawia mwenzake alicho nacho na afanye hivyo kwa ukarimu. Msimamizi na asimamie kwa bidii; naye mwenye kutenda jambo la huruma na afanye hivyo kwa furaha.
9 Mapendo yenu na yawe bila unafiki wowote. Chukieni jambo lolote ovu, zingatieni jema.
10 Pendaneni kindugu; kila mmoja amfikirie kwanza mwenzake kwa heshima.
11 Msilegee katika bidii, ila muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana.
12 Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida, na kusali daima.