22 Ndiyo maana Mungu alimkubali kuwa mwadilifu.
23 Inaposemwa, “Alimkubali,” haisemwi kwa ajili yake mwenyewe tu.
24 Jambo hili linatuhusu sisi pia ambao tunamwamini Mungu aliyemfufua Yesu, Bwana wetu, kutoka kwa wafu.
25 Yeye alitolewa auawe kwa ajili ya dhambi zetu, akafufuka ili tufanywe waadilifu.