32 “Nani aliye Mungu isipokuwa Mwenyezi-Mungu?Nani aliye mwamba wa usalama ila Mungu wetu?
33 Mungu huyu ndiye kimbilio langu imara,na ameifanya njia yangu iwe salama.
34 Ameiimarisha miguu yangu kama ya paa,na kuniweka salama juu ya vilele.
35 Hunifunza kupigana vita,mikono yangu iweze kuvuta upinde wa shaba.
36 Umenipa ngao yako ya kuniokoa;msaada wako umenifanya mkuu.
37 Umenirahisishia njia yangu;wala miguu yangu haikuteleza.
38 Niliwafuatia adui zangu na kuwaangamiza,sikurudi nyuma mpaka wameangamizwa.