37 Umenirahisishia njia yangu;wala miguu yangu haikuteleza.
38 Niliwafuatia adui zangu na kuwaangamiza,sikurudi nyuma mpaka wameangamizwa.
39 Niliwaangamiza, nikawaangusha chiniwasiweze kuinuka tena;walianguka chini ya miguu yangu.
40 Wewe ulinijalia nguvu ya kupigana vita;uliwaporomosha adui chini yangu.
41 Uliwafanya adui zangu wakimbie,na wale walionichukia niliwaangamiza.
42 Walitafuta msaada, lakini hapakuwa na wa kuwaokoa,walimlilia Mwenyezi-Mungu, lakini hakuwajibu.
43 Niliwatwanga na kuwaponda kama mavumbi ya nchi,nikawaponda na kuwakanyaga kama matope barabarani.