1 “Mnamo mwaka wa tatu wa utawala wa mfalme Belshaza, maono mengine yalinijia mimi Danieli, licha ya maono yale ya kwanza.
2 Katika maono haya, nilijikuta niko Susa, mji mkuu wa mkoa wa Elamu. Nilikuwa nimesimama kando ya mto Ulai.
3 Nilipoinua macho yangu, niliona kondoo dume amesimama kando ya mto huo. Kondoo huyo alikuwa na pembe mbili ndefu, lakini moja ilikuwa ndefu zaidi, nayo ilitokea baada ya ile nyingine.
4 Nilimwona huyo kondoo dume akishambulia kuelekea magharibi, kaskazini na kusini. Hakuna mnyama yeyote aliyethubutu kusimama mbele yake, wala kuzikwepa nguvu zake. Alifanya apendavyo na kujikweza mwenyewe.
5 “Nilipokuwa ninawaza juu ya jambo hili, niliona beberu mmoja kutoka upande wa magharibi akija kasi bila kugusa ardhi. Kati ya macho yake alikuwa na pembe moja kubwa sana.