18 Wazawa wa Yakobo watakuwa kama motona wazawa wa Yosefu kama miali ya moto.Watawaangamiza wazawa wa Esaukama vile moto uteketezavyo mabua makavu,asinusurike hata mmoja wao.Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.
19 Wale wanaokaa Negebu wataumiliki mlima Esau;wale wanaokaa Shefela wataimiliki nchi ya Wafilisti.Waisraeli watamiliki nchi za Efraimu na Samariana watu wa Benyamini wataimiliki nchi ya Gileadi.
20 Waisraeli walio uhamishoni Halawataimiliki Foinike hadi Sarepta.Watu wa Yerusalemu walio uhamishoni Sefaradiwataimiliki miji ya Negebu.
21 Waokoaji watapanda juu ya mlima Siyoniili kuutawala mlima Esau;naye Mwenyezi-Mungu atakuwa ndiye Mfalme.”