8 Mimi Mwenyezi-Mungu nakuuliza hivi:Je, siku hiyo, sitawaangamiza wenye hekima kutoka Edomuna wenye maarifa kutoka mlima Esau?
9 Ewe Temani, mashujaa wako watatishikana kila mtu atauawa mlimani Esau.
10 “Kwa sababu ya matendo maovumliyowatendea ndugu zenu wazawa wa Yakobo,mtaaibishwa na kuangamizwa milele.
11 Siku ile mlisimama kando mkitazama tu,wakati wageni walipopora utajiri wao,naam, wageni walipoingia malango yaona kugawana utajiri wa Yerusalemu kwa kura.Kwa hiyo nanyi mlitenda kama wazawa wao.
12 Msingalifurahia siku hiyo ndugu zenu walipokumbwa na mikasa;msingaliwacheka Wayudana kuona fahari wakati walipoangamizwa;msingalijigamba wenzenu walipokuwa wanataabika.
13 Msingeliingia katika mji wa watu wangu,siku walipokumbwa na maafa;msingelipora mali zao, siku hiyo ya maafa yao.
14 Msingelisimama kwenye njia pandana kuwakamata wakimbizi wao;wala msingeliwakabidhi kwa adui zaowale waliobaki hai.