1 Usiku nikiwa kitandani mwangu,niliota namtafuta nimpendaye moyoni mwangu;nilimtafuta, lakini sikumpata.
2 Niliamka nikazunguka mjini,barabarani na hata vichochoroni,nikimtafuta yule wangu wa moyo.Nilimtafuta, lakini sikumpata.
3 Walinzi wa mji walinionawalipokuwa wanazunguka mjini.Basi nikawauliza,“Je, mmemwona mpenzi wangu wa moyo?”
4 Mara tu nilipoachana nao,nilimwona mpenzi wangu wa moyo;nikamshika wala sikumwachia aondoke,hadi nilipompeleka nyumbani kwa mama yangu,hadi chumbani kwake yule aliyenizaa.