2 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
3 ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.
4 Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.
5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.
6 Kwa kuwa imeandikwa katika maandikoTazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima,Na kila amwaminiye hatatahayarika.
7 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini,Jiwe walilolikataa waashi,Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
8 Tena,Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha.Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo.