29 Ni nani aliye dhaifu, nisiwe dhaifu nami? Ni nani aliyekwazwa nami nisichukiwe?
30 Ikinibidi kujisifu, nitajisifia mambo ya udhaifu wangu.
31 Mungu, Baba wa Bwana Yesu, aliye mtukufu hata milele, anajua ya kuwa sisemi uongo.
32 Huko Dameski liwali wa mfalme Areta alikuwa akiulinda mji wa Wadameski, ili kunikamata;
33 nami nikatelemshwa ndani ya kapu, katika dirisha la ukutani, nikaokoka katika mikono yake. e.