2 (Kwa maana asema,Wakati uliokubalika nalikusikia,Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.)
3 Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe;
4 bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida;
5 katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga;
6 katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki;
7 katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;
8 kwa utukufu na aibu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema; kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli;