11 Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee;
12 kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena.
13 Lakini yote yaliyokemewa hudhihirishwa na nuru maana kila kilichodhihirika ni nuru.
14 Hivyo husema,Amka, wewe usinziaye,Ufufuke katika wafu,Na Kristo atakuangaza.
15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.
17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.