Flp.
Sura 2:15-21
Swahili Union Version
15mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,
16mkishika neno la uzima; nipate sababu ya kuona fahari katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala sikujitaabisha bure.
17Naam, hata nikimiminwa juu ya dhabihu na ibada ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote.
18Nanyi vivyo hivyo furahini, tena furahini pamoja nami.
19Walakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu.
20Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli.
21Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu.